BREAKING NEWS

Advertise Here

Friday, January 20, 2017

Memphis depay atua rasmi lyon


Winga wa Kiholanzi Memphis Depay amesaini mkataba kujiunga na klabu ya Ufaransa Olympique Lyon baada ya kukosa ushawishi kwenye kikosi cha Mourinho
Klabu ya Ufaransa Lyon imetangaza kuwa imekamilisha usajili wa Memphis Depay kutoka
Manchester United .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amemwaga wino kusaini dili la paundi milioni 16 na United wameweka kifungu kichowaruhusu kumnunua endapo watamhitaji.
Akithibitisha habari hizo kupitia mtandao wa Twitter, Depay alilipa fadhila kwa wachezaji wenzake wa United, akimwelezea nahodha Wayne Rooney kama “gwiji” na amesema mara zote amejihisi salama akiwa na David De Gea.
Aliongeza: “Shukrani kwa kumbukumbu zote za nyakati zangu nikiwa na Mashetani Wekundu. Sitasahau kamwe ushirikiano wenu katika United”
Akizungumzia kuondoka kwa Depay mchana huu, meneja wa United Jose Mourinho aliwaambia maripota: “Alikuwa mchezaji mahiri mwenye kiwango kikubwa, kwa hiyo kama mtu anadhani anaondoka kwa sababu si mchezaji mwenye kiwango, ni makosa makubwa.
“Kama naweza kupata sababu, naweza kusema anaondoka kwa sababu namba yake ina ushindani mkubwa. Yeye ni winga na mawinga ndio wachezaji wengi tulio nao. Ni vigumu kupata nafasi mara zote, na si rahisi kukubali kuwa chaguo la pili, kwa sababu ni eneo ambalo hatuna shida.”
Depay alijiunga na United ikiwa chini ya Louis van Gaal mnamo 2015 akitokea PSV kwa ada ya awali ya paundi milioni 25 lakini amecheza mara nne tu, tena akitokea benchi katika kikosi cha Mourinho.

Share this:

 
Copyright © 2014 MBONDA. Template Designed by OddThemes - Videopiar