Watumishi wa kata ya mtimbira waibuka mabingwa kombe la vitongoji Cup

Hatimaye Timu ya watumishi ya Kata ya mtimbira wameibuka mshindi Wa mashindano ya ligi ya vitongozi Cup.
Timu ya watumishi Wa Kata ya mtimbira imeibuka mshindi Wa kombe la vitongoji Mara baada ya kukifunga kitongoji cha kirungwili Kwa jumla ya magoli 3-1.
Katika mashindano hayo yaliyoanzwasha na Elias ndaminagani (kadunu) mshindi Wa kwanza amepata ng'ombe huku mshindi Wa pili akipata mbuzi.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wananchi wamewataka wafadhili wengine kujitokeza kuanzisha ligi katika Kata yao.
"Ndugu mwandishi siujua mwezi huu hadi Wa kumi na mbili atuna kazi ya kufanya hivyo kama atatokea mtu kuanzishwa ligi itakuwa vizuri maana pia itawawezesha vijana kujiepusha na makundi mabaya"

No comments