BREAKING NEWS

Advertise Here

Monday, May 14, 2018

Kampuni tisa zafutiwa usajili.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama amemuagiza kamishna mkuu wa kazi nchini kuzifutia usajili kampuni tisa za wakala binafsi wa ajira kwa  kosa la kubadili anauani za ofisi zao bila kutoa taarifa kwa kamishina wa kazi na kuto wasilisha taarifa kwa kamishna wa kazi mara baada ya mikataba ya kazi ya wafanya hao kukamili.

Aidha Waziri Mhagama amemuagiza kamishna wa kazi kuzifanyia uhakiki wakala zote zinazoendesha shughuli za wakala binafsi za huduma za ajira nchini ili kuona kama wanatekeleza na kuzingatia matakwa ya sheria ya huduma ya ajira namba 9 ya mwaka 1999 na kanuni zake kupitia tangazo la serikali namba 232 ya mwaka 2014.

Waziri Mhagama amesema amechukua uamuzi huo mara baada ya kubaini uwepo wa udanganyigu mkubwa wa  mawakala  hao na kuelekeza shughuli hiyo ifanywe na wakala wa huduma za ajira wa serikali wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuangalia namna ya kuingia mikataba na nchi husika ili kuwa na uhakika na Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi wananufaika.

Waziri Mhagama ametumia nafasi hiyo kuwataka wale wote ambao walikuwa wamesajiliwa na kampuni hizo kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi kutoa taarifa haraka kwenye mamlaka husika ili waweze kupewa maelekezo na utaratibu mwingine unaostahili.

Kadhalika Waziri Mhagama amemuelekeza kamishana huyo wa kazi nchini kuendelea kufuatilia ukweli wa Watanzania  4,118 waliounganishwa na fursa za ajira nje ya nchi ili kujua mahali walipo, mikataba yao na ustawi wao huku ikidaiwa kuwa wasichana 3,706 walioajiriwa nje ya nchi.

Share this:

 
Copyright © 2014 MBONDA. Template Designed by OddThemes - Videopiar